Msimu mpya wa Fema TV Show!

created by Bahati Mdetele Nyembe |

Ule Mdundo wa Fema TV Show umerejea rasmi kurindima kwenye luninga yako! Ni msimu wa 12 ambao utaangazia safari mahiri ya miaka 20 ya Femina Hip katika mihimili yake iliyojikita katika Elimu ya haki na afya ya uzazi na ujinsia, Uwezeshaji kiuchumi na Ushiriki wa wanajamii katika masuala ya uraia! Jiweke sawa kwa vishindo vya Kucheza Salama, Kuruka Juu na zaidi Kusema na Fema!!! Jiandae kuwashuhudia wadau mbalimbali waliowahi kuzipamba kurasa za Fema na mazao yake akiwemo Stara Thomas, Rashid Matumla, Madame Ritha, Yvone Sherry almaarufu Monalisa, Shubert na zaidi aliyekuwa mtangazaji wa kwanza wa Fema TV Show Lydia Igarabuza! Hakika si msimu wa kukosa ukishereheshwa vyema na Elimu Burudani…

Ni kuanzia Jumapili hii Machi 10, 2019 na Kila Jumapili saa moja kamili jioni, together tukiwakilisha ndani ya EATV (East Africa Television) na Marudio ni kila Jumatano saa nane na nusu mchana…USIKOSE MDUNDO HUU!!!

#20YaKibabe