Local traditions and customs

created by Fema Team |

Ya Kiswahili iko chini — A wise man once said, “A people without knowledge of their past history, origin and culture, is like a tree without roots.” And that is what makes this issue of Fema so important!

In this issue, we are covering local customs and traditions. Where do you come from? What were you taught? Think back to when you were younger; did you get a chance to hear your grandmother or grandfather tell stories? How did that happen, what stories did they tell you? What food did you eat and how was it cooked? What of funerals, weddings, puberty and other rituals; how were these celebrated? All these and more, make up our local customs and traditions, and in this issue, we wanted to dive in and cover as much as we can, about Tanzania’s local customs and traditions!

Our Cover Story is of Isack Abeneko, a young Tanzanian musician and dancer. He loves local music! From his performances, Abeneko hopes that youth whose inspiration is limited to culture beyond their own, can realize how beautiful our own music is! It is his dream that Tanzania grows to appreciate its own musical heritage. Learn more about him on page 3!

We go on a tour with our Sema Tenda as it takes us on a journey to the various museums we have in Tanzania! Oh, what a sight! All the structures, the old ways of life, the stories that each different ornament tells! 
It’s like another lifetime! You’re right! It was! It was the life our parents and grandparents lived in! So different from how we live now. 
Be sure not to skip this one!

Grandmothers always have the best stories! And our Story Yangu is no different. Here we meet our beloved Bibi Mtetwa Binti Simba, and we listen attentively as she takes us back to the old days, narrating all the entertaining things she experienced growing up. She was so amusing! 
We couldn’t stop listening to her and we are sure you won’t too!

The cartoon story is a must read! Buda and Boya need to keep in touch after Standard VII, but there are no mobile phones! No Facebook, Twitter, Instagram or anything of that sort! How do they do it? Turn to page 46 and you’ll find out! 

In this issue, you won’t only learn about your own customs and 
traditions, but those of others too! Last but definitely not least, Femina has a new Leadership! 
Read on and find out who they are!

Enjoy!

------------------

Mtu mmoja mwenye busara aliwahi kusema, "Watu wasiofahamu historia yao, asili na utamaduni wao, ni kama mti usio na mizizi." Na hilo ndilo linalifanya toleo hili la Fema kuwa muhimu sana!

Katika toleo hili, tunaangazia tamaduni, mila na desturi zetu. Unatokea wapi? Ulifundishwa nini? Jikumbushe kidogo, enzi zile uko bado mdogo; ulipata nafasi ya kumsikia bibi au babu yako akisimulia hadithi? Ilikuwaje, walikusimulia hadithi gani? Mlikuwa mnakula misosi gani na ilipikwaje? Vipi kuhusu misiba, harusi, kubalehe na mila nyingine, zilisherehekewaje hizi? Haya yote na mengine, yanaunda tamaduni, mila na desturi zetu, na katika toleo hili, tulitaka kutazama kwa kina mambo mengi iwezekanavyo juu ya utamaduni na mila za kitanzania!

Stori inayolibeba toleo hili ni ya Isack Abeneko, mwanamuziki kijana na dansa wa Kitanzania. Anapenda muziki wa nyumbani! Kutokana na maonyesho yake, Abeneko anatumai kuwa vijana ambao mapenzi yao ya muziki yanalalia zaidi kwenye vionjo vya tamaduni za nje ya nchi, watagundua utamu wa muziki wetu wenyewe. Ni ndoto yake kwamba Tanzania itafikia hatua ya kuuenzi urithi wake wa muziki. Pata zaidi ukurasa wa 3!

Tunakwenda kwenye ziara na Sema Tenda yetu, inatupeleka kwenye safari ya makumbusho mbalimbali tulizonazo Tanzania! Lo, burdani! Stori za mambo ya kale, mitindo tofauti ya maisha, hadithi zilizomo katika vitu vilivyohifadhiwa humo, dooh, ni kama maisha mengine kabisa! Ni maisha ambayo wahenga wetu mabibi na mababu wa miaka hiyo waliishi. Tofauti sana na jinsi tunavyoishi sasa. Yaani usipite bila kuisoma hii!

Bibi siku zote huwa na hadithi bora! Katika Stori Yangu tunakutana na bibi yetu mpendwa, Bibi Mtetwa Binti Simba. Tunamsikiliza kwa makini akiturudisha siku za zamani, akisimulia mambo yote ya burudani aliyopitia akikua. Alituvunja mbavu kwa vichekesho vyake! Tulimsikiliza bila kuchoka na tuna hakika hata wewe utanaswa na simulizi yake!

Hadithi ya picha sasa, unaikosaje? Buda na Boya wanahitaji kuwasiliana baada ya Darasa la Saba, lakini hakuna simu za mkononi! Hakuna Facebook, Twitter, Instagram wala chochote kingine cha aina hiyo! Wanafanyaje? Fungua ukurasa wa 46 umalizie mwenyewe!

Katika toleo hili, hautajifunza juu ya mila na desturi zako tu, utajifunza na za wengine pia!
Mwisho lakini sio umuhimu; Femina ina uongozi mpya! Ni akina nani, watafanya nini, majibu yote yamo ndani.

Pata uhondo.
 

Read/Soma PDF