Body Concerns and Curiosities - Part 2

created by Fema team |

Ya Kiswahili iko chini — Hello readers! It’s another education packed issue of Fema Magazine! This quarter, we partner with UNFPA to discuss various topics that affect our Sexual Reproductive Health and Rights (SRHR), such as maternal mortality, HIV/AIDS, gender-based violence, safe sex and so much more! Are you excited? We hope so! So, let’s jump right in!

We start off with a gripping Cover story! Can you imagine having your whole life turned upside down in just a few minutes? Everything you had been planning for almost a year, falling apart and crashing? Well, that’s exactly what happened to Michael Omwony, our cover story, who shares with us what was the absolute best day of his life, as well as the worst day of his life! Turn to page 4 and find out what happened on that day!

What would you do if someone offered to take all your troubles away! Sounds like a chance of a lifetime, right?! Well! that’s what it seemed like for Ngeta. But alas! She got more than she bargained for, and at the end of it all, it didn’t seem worth it. What do we mean? Ruka Juu will tell you.

In our ChezaSalama article, we are taken through a journey to help us understand what safe sex is. We are also challenged; fikiri kabla ya kutenda (think before you act), we are encouraged. There are many questions to be asked and many answers too. But read it all in this section. Nothing beats the wise words from Bibi, and here, we would like to take you back a little – to our issue 58 on Body Concerns and Curiosities! Do you remember it? Do you remember how we talked about puberty and everything that came with it? 

Well, Bibi has something to say too. What is she saying? Well, let’s find out in Dondoo za Bibi. We bet you’re excited now!
So! dig in!

-----------------------------

Mambo ni vipi? Fema toleo jipya hili hapa live bila chenga! Kama kawa kama jadi limesheheni elimu na burudani. Tumepiga collabo na UNFPA kujadili mada mbalimbali zinazohusu afya yetu ya uzazi pamoja na haki zinazoambatana nayo. Vifo vitokanavyo na uzazi wakati wa kujifungua ni mojawapo, lakini pia tunazungumzia VVU/UKIMWI, udhalilishaji wa kijinsia, ngono salama na mengine mengi! Tuko pamoja? Twende kazi.

Tuanze na simulizi inayogusa hisia kwa namna ya pekee; iko kwenye cover story! Pata picha maisha yako yanapinduliwa kisebe mnebe ndani ya dakika chache tu? Kila kitu ambacho ulikipanga na kufanya kwa takriban mwaka mmoja kinaanguka na kuharibika kabisa. Hakika, hicho ndicho kilichomtokea Michael Omwony. Michael anatushirikisha siku njema sana na siku mbaya za maisha yake. Fungua ukurasa wa 2 twende sawa.

Utafanya nini iwapo atatokea mtu ajitolee kuyabeba matatizo yako yote na kuyashughulikia? Kama ndoto eeh, si ndio? Basi ndivyo ilivyokuwa kwa Ngeta. Lakini daah! Alipata zaidi ya alichokikusudia, na mwisho wa yote, hakikuwa na ile thamani aliyoitarajia. Hapa namaanisha nini? Ruka Juu itakueleza yote.

Katika makala ya ChezaSalama, tunapelekwa katika safari itakayotusaidia kuelewa ngono salama ni nini. Tunapewa changamoto ya kufikiri kabla ya kutenda. Yapo maswali mengi na majibu pia yapo. Usikose kujielimisha hapo.

Hakuna maneno matamu na yenye busara kama nasaha za bibi, na hapa niruhusu  nikurudishe nyuma kidogo mpaka toleo la 58 linalohusu Body Concerns and Curiosities. Je, unalikumbuka? Unakumbuka jinsi ambavyo tulizungumza kuhusu balehe na yote yanakuja nayo? Bibi nae ana jambo lake anakazia humo. Ya nini nikumalizie utamu? Kamsikilize mwenyewe kwenye Dondoo za Bibi.

Bila shaka sasa uko tayari kuchimba zaidi,
Kazi kwako!
 

Read/Soma PDF