CHIMBUKO LA SIKU YA "MTOTO WA AFRIKA" JUNI 16 KILA MWAKA

CHIMBUKO LA SIKU YA "MTOTO WA AFRIKA" JUNI 16 KILA MWAKA-blog-image

Ushiriki wa Shirika la Siri la Afrikaner Broederbon katika Mauaji ya Soweto

Leo ni tarehe 16 Juni 2023, miaka 48 sasa tangu risasi ilipoingia barabara mwilini mwa mwanafunzi Zolile Hector Pieterson huko Soweto, Afrika Kusini. Ingawa yeye si pekee aliyefariki (wapo wengine pia) lakini picha yake iliyopigwa na mwandishi aliyejibanza pembeni ya gari lake dogo ilisambaa haraka kote duniani.

Zolile alizaliwa mwaka 1963 pamoja naye wapo ndugu zake wawili wa kuzaliwa nao akiwemo dada yake Antoinette Sithole ambaye huyu wa upande wa kushoto pichani akionekana kulia kwa uchungu akiona kuwa mdogo wake hana maisha tena! Wahenga husema damu ni nzito kuliko maji, lakini fahamu kuwa kuna uji nao ni mzito kuliko maji, kuna mafuta ya kulainisha mashine nayo ni mazito kuliko maji na kuna juisi ya matunda nauo ni nzito kuliko maji, aaah, vingi mno. Lakini vyote hivyo hata ukivijumlisha pamoja havifikii utizito wa thamani ya damu ya binadamu!

Mapema asubuhi ya tarehe 16 Juni 1976 katika shule moja mjini Soweto, Afrika Kusini, wanafunzi waliandamana kudai mabadiliko ya mtaala ili yaendane na hali halisi ya maisha yao baadae ikiwemo lugha ya kufundishia. Wanafunzi walidai lugha ya kufundishia iwe inayoeleweka kwa wanafunzi wote na jamii ypte yaani lugha ya Afrikaans badala ya Kiingereza pekee.

Polisi wakati huo walifika eneo la tukio na kuanza kumimina risasi bila kujali itatua kwa nani. Ni vile walikuwa wanatekeleza “amri kutoka juu”. Wanafunzi walianza kutawanyika kwa lazima ili kujiokoa. Wakati huo kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Mbuyisa Makubo alikuwa amewakusanya wadogo zake wa hiyari, Zolile na Antoinette. Inaelezwa kwamba walikuwa majirani walikokuwa wanaishi, basi ilikuwa ni desturi yao kwenda shuleni pamoja na kurudi pamoja. Ujirani wao uliunganisha mioyo yao kwa utu na kuthaminiana wangali wadogo. Makubo alikuwa kama kaka kwao na walimtazama kama kiongozi wao wawapo shuleni au katika michezo na watoto wengine.

Other Blogs

View All
Kuwa na ndoto, ifukuzie, itimize.-blog-image

Kuwa na ndoto, ifukuzie, itimize.

Published At Nov. 23, 2024

Read More
CHIMBUKO LA SIKU YA "MTOTO WA AFRIKA" JUNI 16 KILA MWAKA-blog-image

CHIMBUKO LA SIKU YA "MTOTO WA AFRIKA" JUNI 16 KILA MWAKA

Published At Jun. 18, 2024

Read More
Femina Hip Yatambuliwa kwa Kuipambania Hedhi Salama-blog-image

Femina Hip Yatambuliwa kwa Kuipambania Hedhi Salama

Published At May. 23, 2024

Read More

Ready to be a part of something bigger?

Be the Change. Join the Movement.

Join Femina Hip and help us drive change, challenge stereotypes, and empower youth. Together, we can create a more equitable and inclusive world. Your support matters. Start your journey with us today.

Join Us
femina-logo

Copyright © 2025 All Rights Reserved.

Call:+255 22 270 0742/3

Email: info@feminahip.com

SMS Number:+255 75 300 3001

23 Migombani St, Dar es Salaam, Tanzania.

Google Maps

Be the first to get the latest news about us, including blogs and so much more.

By subscribing you accept the Privacy Policy.

Designed & Developed By iPF Softwares